Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Tawi la Dar es Salaam, Daimon Malaki, akitoa mfano namna ya kupanda Mnara kwa wafanyakazi wenzake kutoka idara mbalimbali za kampuni hiyo wakati wafanyakazi hao walipofanya ziara ya mafunzo ya siku moja kwenye minara mbalimbali ya kampuni hiyo pamoja na kufanya usafi katika maeneo yanayozunguka minara ya kampuni hiyo.
Kuendelea
kuwepo kwa kampeni mbalimbali zinazolenga kuboresha usafi wa mazingira
na miundombinu kumeendelea kuwaamsha wadau na taasisi mbalimbali
kuendelea kuunga mkono jitihada hizo, ambapo kampuni ya mawasiliano ya
Halotel imezindua kampeni ya wafanyakazi wake kufanya usafi katika
maeneo yote yanayozunguka minara iliyojengwa na kampuni hiyo.
HALOGREEN,
ndio jina la kampeni ambayo ina lengo la kuboresha mazingira
yanayozunguka maeneo yaliyojengwa minara ya kampuni hiyo ya Simu.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika eneo la ubungo maji, jijini
Dar es Salaam, ambapo kuna moja ya minara ya Halotel, Meneja Uhusiano wa
Kampuni hiyo, Stella Pius, amesema kampeni hiyo ina lengo la kuweka
mazingira safi na salama kwenye maeneo yote ambayo imewekwa mitambo ya
mawasiliano.
“Tunathamini
umuhimu wa kutunza mazingira, Minara ya mawasiliano tuliyo ijenga ni ya
teknolojia ya hali ya juu na ni rafiki kwa Mazingira, licha ya hivyo
bado tunaona ni jukumu letu kuhakikisha tunaweka mazingira yanayozunguka
minara yetu katika hali ya usafi,” Alisema na kuongeza.
Wafanyakazi
wote kwa upande wetu tumeona kuna jambo ambalo tunaweza kulifanya
hususan katika kulinda na kuyaweka mazingira yetu katika hali ya usafi
hivyo tumeamua kujitolea kufanya usafi katika maeneo yote yanayozunguka
minara yetu nchi nzima, Alisema Pius.
Pius,
alihitimisha kwa kusema kuwepo kwa Mazingira rafiki na safi katika
maeneo ya minara hiyo ambayo mingine iko katika maeneo ya makazi ya watu
yatawezesha kuwa na jamii yenye afya na inayozingatia usafi wa
mazingira.
Mkuu
wa Ufundi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Tawi la Dar es Salaam,
Daimon Malaki, akiwaeleza wafanyakazi wenzake kutoka idara mbalimbali
za kampuni hiyo namna minara ya mawasiliano ya simu za mkononi
inavyofanya kazi wakati wafanyakazi hao walipofanya ziara ya mafunzo ya
siku moja kwenye minara mbalimbali ya kampuni hiyo pamoja na kufanya
usafi katika maeneo yanayozunguka minara ya kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment