Kuelekea fainali za AFCON2017
Mataifa 8 kati ya 16 yatakayoshiriki michuano ya 2017 yamewahi kushinda Ubingwa wa Afrika.
1. Algeria ‘The Desert Warriors’
Taifa analotoka mchezaji bora wa Afrika na EPL - Wameshinda taji moja katika michuano 17 waliyoshiriki-1990
2. Cameroon ‘The Indomitable Lions’
Wameshinda mataji manne katika michuano 16 waliyofuzu - 1970, 1984, 2000 na 2002
3. DRC ‘The Leopards’
Wameshinda mataji mawili katika michuano 15 waliyoshiriki- 1968 na 1974
4. Tunisia ‘Eagles of Carthage’
Wameshinda mara moja katika michuano 16 waliyoshiriki, ilikuwa 2004 michuano hii ilipofanyikia kwenye ardhi yao.
5. Morocco ‘Atlas Lions’
Taifa lingine la kiarabu ambalo limeshinda taji moja katika mara 15 walizowahi kufuzu, ilikuwa mwaka 1976.
6. Ivory Coast ‘The Elephants’
Kizazi chao cha dhahabu kilishindwa kutwaa taji hili lakini kwa sasa ndio mabingwa watetezi baada ya kulitwaa taji hili mwaka 2015. Pia waliwashawahi kutwaa taji hili mwaka 1992, wameshiriki mara 21.
7. Ghana ‘Black Stars’
Hii ndio timu ambayo imecheza fainali nyingi zaidi za AFCON katika historia, wameshiriki michuano hii mara 20, na pamoja na kufanikiwa kufikia hatua ya final mara nyingi wameambulia makombe 4 - 1963, 1965, 1978 na 1982
8. Egypt ‘The Pharaohs’
Mafarao ndio timu inayoongoza kufuzu mara nyingi kushiriki michuano hii - wamefuzu mara 22 na pia ndio Taifa linaloongoza kutwaa taji hili mara nyingi, wamebeba mara 7 - 1957, 1959, 1086, 1998, 2006, 2008 na 2010.
Mashindano yanaanza kesho Januari 14 na yatafikia kilele Februari 5
No comments:
Post a Comment