HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 15, 2016

TIC YATEMBELEA MAENEO YA UWEKEZAJI WA VIWANDA, MKOANI PWANI

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Cliford Tandari (kulia) akisaliama na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng wakati alipotembea eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza "Tiles" Desemba 14, 2016 lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. TIC ilitembelea eneo hilo, ikiwa ni utaratibu wake iliyojiwekea wa kuwatembelea wawekezaji wote nchini na kuona maedeleo ya uwekezaji walioomba kama unafanyika kama walivyoomba. Ujenzi wa kiwanda hiki unatarajiwa kuanza mapema mwezi Januari 2017 na zaidi ya Watanzania 6000 wataweza kupata ajira kupitia kiwanda hiki. Kabla ya kutembelea mradi huo, Tandari aliembatana na baadhi ya watendaji wa TIC alitembelea eneo lingine linalotarajiwa kujengwa kiwanda cha kutengeneza sabuni, kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Cliford Tandari akifafanua jambo kwa waandishi wa harabi (hawapo pichani) wakati alipotembelea eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza "Tiles" Desemba 14, 2016 lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng akieleza jambo mbele ya wanahabari pamoja na Ujumbe wa TIC wakati wa ziara ya kutembelea eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza "Tiles" Desemba 14, 2016 lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.


 Muonekano wa eneo hilo ambalo sasa linawekwa sawasawa tayari kwa maandalizi ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kutengeneza "Tiles"hapa nchini.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad