
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwimbaji Lissu alisema kuwa maandalizi yameshakuwa tayari anawaomba Watanzania na wapenzi wa Muziki wa Injili kumuunga mkono ili kuhudhuria katika uzinduzi huo. Mwimbaji John Lissu aliongeza kuwa waimbaji wote wamefanya mazoezi ya kutosha hivyo mwenye shughuli ambaye ni (Yesu) anasubiri watu wakife siku hiyo ili aanze kazi yake. Waimbaji watakao msindikiza John Lisu ni Pastor Safari Paul, Cosmas Chidumule, Glorious Celebration, Bomby Johnson, The Voice na Next Level. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huwa Media, Bw. Jacob alisema kuwa kila kitu kimesha kamilika kuanzia vyombo vya Muziki, muonekano wa Ukumbi na pia alitoa rai kwa watu wote kuwahi kwani saa nane kamili shughuli nzima itaanza. Ni Tarehe 3/2/2012 katika ukumbi wa CCC Upanga kwa kiingilio cha sh 5000/=.Muda ni Saa nane (8) Mchana.
Mwimbaji Mercy Masika kutoka nchini Kenya akiongea machache.
Mwimbaji Angel Bernard akiongea machache.
No comments:
Post a Comment