
Timu ya Kagera Sugar, Wanamkurukumbi wawameanza kupiga jalamba kwenye Uwanja wa Kaitaba kwa mara ya kwanza Tangu Uwanja huo ukamilike hivi karibuni kwa ukarabati murua uliofanywa. Uwanja huo sasa uko tayari kwa Michezo mbalimbali ikiwemo Mitanange ya Ligi Kuu Vodacom. Kagera Sugar wanajifua uwanjani hapo ikiwa ni uwanja wao wa nyumbani kujiandaa kwa Mchezo wao wa tarehe 3 Septemba, 2016 dhidi ya Mwadui kutoka Shinyanga ambapo nmchezo huo utapigwa katika Uwanja huo ambao umejengwa kwa Viwango vya Fifa.
‘Wanankurukumbi’ walipambana hadi siku ya mwisho kukwepa mkasi wa kushuka daraja msimu uliopita wakiwa na kocha wao Adolf Rishard na sasa wakiwa na Kocha mpya msimu huu mpya 2016/2017 Mecky Mexime ambao pia wamefanya usajili wa nguvu wakiwemo makipa. Leo wameanza kujifua kwenye Uwanja wao kwa ajili ya kuhakikisha hawakumbwi na gharika iliyowakosa msimu uliopita na hatimae kufanya vyema kwa msimu huu ambao umeanza kwa aina yake wakianzia ugenini mechi zao mbili za mwanzo.

Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar.














Makipa wa Kagera Sugar wakijiuliza jambo leo wakati wa mazoezi yao kwa mara ya kwanza tangu Uwanja huo umalizike kujengwa hivi karibuni. Kagera Sugar wanajiandaa na Mchezo wao wa Ligi kuu Vodaom tarehe 3.




No comments:
Post a Comment