Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (kulia) akifuatilia mada katika semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Gerald Jeremia akiwa katika semina hiyo LEO. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha akisikiliza jambo kwenye semina hiyo.
Msimamizi
wa Ushauri na Utafiti (PSPTB), Amos Kazinza akitoa mada LEO katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni Mkuu wa Idara ya Ugavi,
Pindani Nyalile akiwa kwenye semina hiyo. Semina hiyo imelenga kutoa
mafunzo kwa watendaji wa MNH ili waweze kuzingatia taratibu na sheria za
manunuzi. Wakurugenzi na wakuu wa idara wa MNH wametakiwa kutoa haki
wakati wa kutoa zabuni. Pia, wameshauriwa kutonunua bidhaa zilizopo
chini ya kiwango.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
No comments:
Post a Comment