Tuesday, July 26, 2016

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora akabidhi vifaa vya michezo kwa vijana wa Kata Nne Manispaa ya Tabora

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora (CHADEMA), Hawa Subira Mwaifunga (katikati) akiambatana na ujumbe wake wakati wakielekea kwenye Uwanja wa Chipukizi, kulikofanyika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Michezo kwa vijana wa Kata nne za Manispaa ya Tabora, iliyofanyika leo Julai 26, 2016. Kata hizo ni Ndevelya, Ifucha, Isevya na Mtendeni.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora (CHADEMA), Hawa Subira Mwaifunga akimkabidhi mlezi wa Timu Kata ya Ifucha, Moses Singo,wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Michezo kwa vijana wa Kata nne za Manispaa ya Tabora, iliyofanyika leo Julai 26, 2016.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora (CHADEMA), Hawa Subira Mwaifunga akimkabidhi vifaa vya Michezo Mwenyekiti wa Bawacha kata ya Ndevelwa, Mariam Ramadha, kwa ajili ya Vijana wa Kata yake.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora (CHADEMA), Hawa Subira Mwaifunga akionyesha uwezo wake wa kusakata kabumbu mbele ya vijana wa Kata nne za Manispaa ya Tabora mara baada ya kuwakabidhi vifaa mbali mbali vya Michezo.

No comments:

Post a Comment