HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 1, 2015

Balozi Njoolay akabidhi barua ya pongezi kwa Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafu Muhammadu Buhari

Tarehe 28 Aprili 2015 Balozi wa Tanzania, Nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay, alimkabidhi Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafu Muhammadu Buhari, barua ya pongezi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete. 

Rais Mteule Jenerali Buhari alimshukuru Rais Kikwete kwa salamu hizo na kukiri kwamba alikwishapokea simu ya pongezi kutoka kwake mara tu baada ya matokeo kutangazwa. Wakati wa mazungumzo yake na Balozi Njoolay, Generali Buhari aliisifu Tanzania kwa kudumisha amani na utulivu na kusema kuwa anaamini kwamba Tanzania itaendelea kuwa kitovu cha amani na utulivi Barani Afrika. Imetolewa na Ubalozi Tanzania, Abuja
Balozi wa Tanzania, Nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay (kulia) akimkabidhi Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafu Muhammadu Buhari, barua ya pongezi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi wa Tanzania, Nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafu Muhammadu Buhari, mara baada ya kukabidhi barua ya pongezi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad