HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 13, 2014

kamati ya nidhamu ya TFF yampa adhabu ya Kifungo Mwanasheria Ndumbaro,Yamfungia Miaka saba ya kutojihusiusha na soka

Na Ripota Maalum,Dar
MWANASHERIA wa klabu  14 zinazoshiriki  Ligi Kuu Tanzania Bara, Damas Ndumbalo ametupwa jela kwa miaka saba kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi na kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mwanasheria huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba, amekumbwa na balaa hilo kufuatia taamko lake alilolitoa wiki mbili zilizopita la kupinga makato ya asilimia 5 kutoka kwa mdhamini wa ligi ambao ni Vodacom pamoja na Azam TV.

Akizungumza katika kutoa hukumu hiyo, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jerome  Msemwa alisema kilichomuhuku Ndumbaro ni kitendo chake cha kutaka kubadilisha maamuzi ya kamati ya utendaji ya TFF bila kuthibitishwa na wajumbe wa Bodi ya Ligi na kukubaliana. Kupingana maamuzi ya kamati ya utendaji ni kosa la kinidhamu.

Alisema kosa lengine alilofanya ni kukimbilia kwenye  vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo litokee, akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa Shirikisho, Malinzi.

“Ndumbaro amehukumiwa kutokana na makosa hayo na kama angezungumza kwa niaba ya klabu basi adhabu hiyo ingekwenda kwao, lakini yeye alijizungumzia tu kama vile alivyotaka iwe,”alisema Msekwa.

Makamu huyo aliyeongozana na Mkurugenzi Msaidizi wa uwanachama, Eliud Mvela  alisema wamemfungia Ndumbaro kwa sababu amekanwa hadharani na vilabu vya Coastal Union, Stend United.

 “Ndumbaro alizungumza kama wakili wa klabu za ligi kuu ila tulipoulizwa  amekanwa ‘ hadharani’ na vilabu huku vikisema kuwa ‘ havikumtuma’ kuzungumza yale ambayo alisema mbele ya vyombo vya habari. Klabu zimesema alizungumza kwa ‘ utashi’ wake mwenyewe, na si wao walimtuma,”alisema Msemwa.


Makamu huyo alisema kufuatia makosa hayo, Ndumbaro amefungiwa kwa mujibu wa kanuni ya  ligi kuu ibara ya 41(6) imemfungia miezi 12 kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi huku ibara ya 41(16) imemfungia kutojihusisha na shughuli zozote za soka kwa miaka saba.

Alisema mbali na hilo Ndumbaro pia alivunja udhamini wa Ligi kati Azam na Vodacom, sambamba na kuisemea serikali, Chama cha Mapinduzi (CCM) na vilabu 14 ambapo adhabu yake kwa mujibu wa kanuni ya Ligi ibara ya 41 (6) amezuiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha miaka saba.

Msemwa alisema katika kikao hicho cha kutoa hukumu Ndumbaro aliwakilishwa na mwanasheria wake Nestor Wandiba ambaye hakuweza kutoa utetezi wowote ila anaruhusiwa kukataa rufaa kwenye kamati ya nidhamu ya rufaa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad