Mkali wa Bongo Flava Tanzania Diamond Platnumz amepewa nafasi ya kushirikiana na Mziiki
kama Brand Partner. Msanii huyu ambaye amefanikiwa kushinda tuzo mbalimbali amekuwa wa
kwanza kutia saini kama Brand Partner na tayari ni mmoja wa mamia ya wasanii pekee wa Afrika
walio katika program ya muziki unaopendwa zaidi Afrika kupitia simu za kiganjani pamoja na kuwa
mwakilishi wa bidhaa hiyo akiwakilisha nchi yake.
"Tunafurahi kwamba Diamond Platnumz kwa sasa ni Brand Partner wa Mziiki," anasema Arun
Nagar, Mkurugenzi Mtendaji wa Spice VAS Africa, watengenezaji wa Mziiki. "Kwa kushirikiana na
msanii mwenye kiwango kama Diamond pamoja na mashabiki wake ni hatua nzuri kwa Mziiki.
Ushirikiano kama huu unaonyesha dhamira yetu ili kuendelea kuhakikisha kwamba watumiaji wetu
na muziki bora wa Afrika unawafikia pale walipo na tutaweza kufanya kazi karibu na Diamond na
kupanua wigo wa wateja wetu na kuwapatia mashabiki wake zaidi ya kile walichotarajia. Nadhani
pia ni ushahidi wa ukweli kwamba sisi tumechukua nafasi kubwa katika ulimwengu wa muziki
streaming na wapenzi wa muziki wa Afrika wanapaswa kukumbuka hilo. "
Mziiki ni huduma pekee inayokupa Miziki ya kiafrika kupitia Streaming, huduma ambayo inatoa
safu mbalimbali ya muziki kutoka Afrika na kimataifa. "Mimi nimepata mzuka kujiunga na Mziiki,"
anasema Diamond. "Programu na simu (mobi) tovuti ni nafasi kubwa kwa ajili ya wasanii kupanua
idadi yao ya mashabiki na kutambulisha mara ya kwanza single yao mpya kusikika bara la Afrika na
dunia."
Mziiki ni programu ya simu iliyoundwa kwa ajili ya Music Streaming iliyosheheni miziki ya Afrika.
Imepata umaarufu haraka ikiwa na mkusanyiko mkubwa wa sauti safi na vipaji kipekee vinavyokidhi
miziki ya kiafrika.Programu hii ni rahisi kutumia,ina makala ambayo huruhusu mtumiaji kushirikisha
marafiki wimbo waupendao au kuwatumia nyimbo kama miito ya simu ya nyimbo walizochagua.
Makala haya yamewekwa kuwawezesha wasanii, kama Diamond, kufikia mashabiki wapya katika
Afrika na duniani kote.
"Mziiki kweli imenipa zaidi ya kile ambacho ningeweza kuomba" Anasema Diamond. "Mimi si tu
kuwapatia mashabiki wangu nafasi ya kupata nyimbo zangu zote bali pia pia kupata nafasi ya
kupanua wigo wa mashabiki wangu kupitia programu ya “Share and Dedicate” .
Wakati mashabiki
wangu wakishirikisha au wakituma wimbo wangu wowote maalum kwa wenzao,nani ajuaye waweza
kusambaa kwa kiasi gani? Mimi tayari nimeshaanza kuona idadi ya mashabiki wangu ikiongezeka
kwa namna hii.
Ikiwa na kiwango kizuri na kuongezeka kwa orodha ya wasanii waliosajiliwa kutoka katika bara la
Afrika, Mziiki ni mahali ambapo wasanii wapya wanaweza kwenda kuzindua kazi zao na wasanii
waliopo sasa kuendelea kukua.
Mziiki ni program ya Mobile Streaming iliyoundwa ili kukidhi mahitaji ya msanii na mashabiki kwa
jumla. Mziiki ilianzishwa mwezi Mei 2014, na imesaidia kuongeza mafanikio katika kazi za wasanii
na inaendelea kukua kila siku na kuwawezesha wasanii kufurahia zaidi kama ilivyo kwa Diamond
Platnumz..
No comments:
Post a Comment