Wakati wa Makuzi yetu enzi zile,ilikuwa ni lazima ukutane na mambo hayo hapo chini hasa katika mchezo wa mpira wa miguu.nayo ni kama ifuatavyo:-
1.Mwenye mpira lazima acheze hata kama hajui kucheza mpira
2.Dogo mnene lazima awe golikipa
3.Mwenye mpira ataamua nani acheze na nani asicheze kwenye mtanange huo.
4.Kama haujashiriki kutafua mifuko ya kutengenezea mpira unaweza usipate namba siku zotee
5.Ukichaguliwa mwishoni ujue uwezo wako ni mdogo kuliko wote kwenye kabumbu.
7.Mwenye mpira anaruhusiwa kubadili golikipa,kama kuna penati imetokea baada ya hapo ataendelea kudaka yule yule.....
8.Mechi itaisha pale giza linapoingia
9.Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka wakati wa mchezo
10.Yule mtaalam wa soka huwa hakosi namba hata siku moja..!
Haya jikumbushe ndugu Mdau na kana unakumbukumbu zozote za aina hii usisite kututumia kupitia Email yetu :
othmanmichuzi@gmail.com
Ukiikumbuka lazima utabasamu tu
No comments:
Post a Comment