Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kupokea msaada wa hundi ya milioni kumi kutoka Zantel kwa ajili ya Chama cha Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) leo jijini Dar es Salaaam, kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu Zantel Bw. Pratap Ghose.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (kulia), Afisa Mtendaji Mkuu Zantel Bw. Pratap Ghose (kushoto) pamoja na viongozi kutoka Chama cha Ngumi Tanzania (BFT) wakiunganisha mikono kwa pamoja kuonyesha ushirikiano wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi Milioni kumi kama msaada kutoka Zantel kwa Chama cha Ngumi Tanzania (BFT).
Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Mutta Rwakatare akitoa shukrani kwa Zantel baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni kumi kuinua mchezo wa ngumi, kushoto ni Katibu Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Makole Mashaga na kulia ni Mjumbe wa Maendeleo ya Wanawake Bi. Aisha George Voniatis. Picha na Genofeva Matemu.
No comments:
Post a Comment