Na Hassan Abbas, Dodoma
Zawadi ya Sh. 10,000 kwa wanafunzi kadhaa walioweza kujitahidi kueleza mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda maana ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ilitosha kuwa kivutio cha aina yake katika ufunguzi wa Wiki ya Elimu uliofanyika leo (Jumamosi) mjini hapa.
Sherehe hizo zilizopambwa kwa burudani mbalimbali kutoka kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na kuhudhuriwa kwa wingi na mamia ya wanafunzi, walimu na wazazi wao ziliakisi uhalisia wa kauli mbiu ya mwaka huu isemayo: “Elimu Bora kwa Wote Inawezekana, Timiza Wajibu Wako.”
Akitumia fursa ya kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo, Waziri Mkuu Pinda aliwaeleza mamia ya wanafunzi na wakazi wa mji wa Dodoma kuwa Mpango wa Matekeo Makubwa Sasa (BRN) ulioanza kutekelezwa na Serikali utasaidia maendeleo ya haraka katika sekta mbalimbali ikiwemo kuinua ubora wa elimu.
Waziri Mkuu alisema Wiki ya Elimu itakayoadhinmishwa nchini kuanzia Mei 3 hadi 10 mwaka huu ikiwa ni mara ya kwanza nchini, itakuwa na lengo la kuwazawadia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliofanya vyema katika mitihani ya mwaka 2013.
“Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa unaotekelezwa katika sekta sita ikiwemo elimu utasaidia sana katika kusukuma mbele juhudi za Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la elimu nchini,” alisema Bw. Pinda.
Kwa mujibu wa Mpango wa BRN moja ya mikakati iliyowekwa kuboresha elimu nchini ni pamoja na kuinua kiwango cha ufaulu kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2015, kuwapatia motisha walimu, kupeleka vifaa vya kuongoza ufundishaji shuleni na kuboresha uwezo wa wanafunzi wa madarasa ya awali katika kumudu stadi za kusoma, kuandika na hesabu.
BRN ni Mpango unaosimamiwa na Kitengo Maalum cha Ofisi ya Rais Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) ukilenga kuweka mfumo unaotekeleza miradi kwa njia za haraka ili wananchi waone matokeo Makubwa na ya haraka.
PDB ilianzishwa Julai, 2013 ambapo mpaka sasa Kitengo hicho kimeweza kusimamia utekeleza wa miradi ya kipaumbele katika sekta sita za elimu, miundombinu, nishati, maji, kilimo na raslimali fedha kwa kasi na matokeo Makubwa kuliko ulivyokuwa utekelezaji kabla ya hapo.
Wiki ya Elimu itafikia kilele Mei 10 mwaka huu ambapo Rais Jakaya Kikwete atatoa zawadi kwa walimu, wanafunzi na shule zilizofanya vyema katika mitihani yao katika sherehe zitakazofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

No comments:
Post a Comment