Mkuu
wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro (katikati) akisisitiza jambo
wakati akifunga mafunzo ya siku 3 kwa maafisa ugani wilaya hapo
yaliyotolewa na TAHA hii leo, kushoto ni mwakilishi wa shirika la TAHA
Bw. Manfred Bitala na kulia ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
wilaya ya Makete Bw. Iddi Nganya.
Miongoni
mwa bwana shamba akizungumzia atakayoyafanya pindi akirudi kwenye eneo
lake la kazi mara baada ya mafunzo hayo kumalizika.
Afisa Mifugo wilaya ya Makete Dr. Nuru Issae akizungumza watakavyopambana na magonjwa ya matunda ya apples.
Bibi Shamba akichangia hoja.
Habari/picha na Edwin Moshi, Makete
Mabwana na mabibi shamba wa kata na vijiji wilayani Makete mkoani Njombe walioshiriki warsha ya siku 3 ya namna ya kuboresha kilimo cha matofaa maarufu kama apples iliyotolewa na shirika la TAHA, wametakiwa kutekeleza kwa vitendo mikakati waliyojiwekea ya namna ya kuboresha zao hilo
Mabwana na mabibi shamba wa kata na vijiji wilayani Makete mkoani Njombe walioshiriki warsha ya siku 3 ya namna ya kuboresha kilimo cha matofaa maarufu kama apples iliyotolewa na shirika la TAHA, wametakiwa kutekeleza kwa vitendo mikakati waliyojiwekea ya namna ya kuboresha zao hilo
Akizungumza
wakati akifunga mafunzo ya siku 3 kwa wagani kazi hao, Mkuu wa wilaya
ya Makete Mh. Josephine Matiro, amerudia kauli yake kuwa suala hilo ni
mkakati wa kitaifa ambao umeagizwa na rais Dk. Jakaya Kikwete, hivyo
mafunzo hayo waliyopatiwa yanatakiwa kutendeka kwa kuwa yana manufaa kwa
wakulima na wananchi wa Makete kwa ujumla
Mh.
Matiro amesema ndani ya muda mfupi anatarajia sifa ya Makete kuwa
inaongoza kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi sasa itabadilika mara moja
na kuonekana kuwa inaongoza kwa kuzalisha matunda ya apples
"Nadhani
mtu ukienda pale Dar es Salaam ama sehemu nyingine ukasema unatoka
Makete tayari wanaelewa kuwa kuna Ukimwi, sasa hilo tunaweza
kulibadilisha, kwa kwenda kuwasaidia wakulima huko mnakotoka, wazalishe
apples kwa wingi kwa kufuata utaalam mliopatiwa na TAHA ili tuone
mabadililo" Alisema Mh. Matiro
Amesema
mikakati waliyojiwekea baada ya mafunzo hayo ni njia nzuri ya
kuifikisha wilaya kule inakotaka kuhusu kilimo cha apples, ambacho
kinatarajiwa kuwa kilimo cha biashara kwa lengo la kuinua uchumi wa
wakulima na wilaya kwa ujumla
Kwa
upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw.
Iddi Nganya amesema wagani kazi hao ndio watekelezaji wakubwa wa
mikakati hiyo na ndiyo maana wakapatiwa mafunzo hayo, hivyo kila mmoja
ana jukumu la kwenda kuitumia ipasavyo kwa wakulima wake
Amesema
tathmini itaonekana hivi karibuni, kwani kipimo cha hayo yote ni kuona
wamebadilishaje kilimo cha wakulima wao huko wanakotoka, kama ikionekana
kuna utofauti itaonekana kuwa mafunzo hayo yameweza kuwasaidia, hivyo
waone jitihada zinazofanywa kuhakikisha mkakati huo unafanikiwa
Naye
Mwakilishi kutoka shirika la TAHA ambaye alikuwa miongoni mwa
mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Manfred Bitala amesema ili kufanikisha
malengo hayo kila mmoja kwa nafasi yake anatakiwa kukubali kubadilika na
kuwajibika ipasavyo kwa nafasi yake
Amesema
wao kama TAHA wanawajibu wao ikiwemo kutoa elimu ambayo tayari
wameshaitoa, na maafisa kilimo hao nao wana nafasi yao na hali kadhalika
na wakulima, hivyo jitihada za vitendo zikifanywa anaimani lengo la
kilimo cha apples kuzaliwa kwa wingi na kwa ubora wa hali ya juu
litafanikiwa
Dk.
Nuru Issae ni Afisa mifugo wilaya ya Makete ni miongoni mwa washiriki
wa mafunzo hayo ambapo amesema jambo watakaloanza kulifanyia kazi mara
moja ni kutambua magonjwa yanayoshambulia apples na kuyatokomeza kwa
kuwa wameelezwa aina mbalimbali za magonjwa yanayoshambulia matunda hayo
Dk.
Issae amesema kabla ya mafunzo haya hawakuwa na wazo kuwa magonjwa
yanaweza kuzorotesha jitihada za mkakati wa kuboresha kilimo cha apple
wilayani hapo, na kwa kuwa wametambua kuwa magonjwa ni kikwazo
kimojawapo, watapambana nayo mara moja
Miongoni
mwa mikakati iliyopangwa baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo ni pamoja
na ufuatiliaji wa magonjwa na kampeni ya pamoja ya kuyatokomeza
magonjwa yanayoshambulia apples, kushirikiana na taasisi mbalimbali na
wadau binafsi wanaolima matunda hayo, kukaa na wakulima na kupanga nao
namna nzuri ya kulima apples kwa manufaa kama walivyoelekezwa na mengine
mengi
No comments:
Post a Comment