Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Idadi ya Watu (UNFPA), Bibi Mariam Khan leo alitembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na kutoa wito kwa serikali kufanya hima katika kukabiliana na changamoto za ongezeko la idadi ya watu na ukuaji wa mijini nchini Tanzania.
Hata hivyo, Bibi Khan alisema kuwa licha ya kuwa ongezeko la idadi ya watu linaathari mbalimbali kama lisipothibiwa, Tanzania inaweza kutuma fursa hiyo kwa kuwekeza kwa vijana kama nguvu kazi kwa shughuli za kimaendeleo ili kuongeza pato na uchumi wa taifa.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa serikali inatambua changamoto hizo, na kuwa kwa sasa inajipanga kuipitia Sera ya Idadi ya Watu ya Mwaka 2006 ili iendane na changamoto hizo.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akiangalia kwa umakini sana takwimu zinazohusiana na masuala ya idadi ya watu nchini Tanzania. Anayemuonesha ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Bibi Mariam Khan (Kushoto).
Mtaalam wa Masuala ya Idadi ya Watu toka UNFPA, Bibi Christine Mwanukuzi-Kwayu (Kushoto) akizungumza wakati alipofuatana na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Bibi Mariam Khan (Kulia) kutembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akizungumza na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Bibi Mariam Khan (hayupo pichani) aliyembelea Ofisi za Tume ya Mipango leo. Pamoja na masuala mengine, walizungumzia changamoto za idadi ya watu na ukuaji wa miji nchini Tanzania. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi Joyce Mkinga.
Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia)
akiangalia takwimu zinazohusiana na masuala ya idadi ya watu nchini
Tanzania. Anayemuonesha ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Bibi Mariam
Khan (Wa pili kulia) aliyembelea Ofisi za Tume ya Mipango leo. Wengine
pichani ni Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya
Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto), Mchambuzi Mkuu wa Sera, Bw.
Edwin Ninde (Wa pili kushoto) na Mtaalam wa Masuala ya Idadi ya Watu
toka UNFPA, Bibi Christine Mwanukuzi-Kwayu.
Naibu
Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi
Florence Mwanri (Kushoto) akifuatilia kwa makini takwimu zinazohusiana
na masuala ya idadi ya watu nchini Tanzania zilizokuwa zikiwasilishwa na
Bibi Mariam Khan (hayupo pichani) alipotembelea Ofisi za Tume ya
Mipango. Kulia ni Mchambuzi Mkuu wa Sera (Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango), Bw. Edwin Ninde.
No comments:
Post a Comment