HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 21, 2014

Safari Lager yawapiga msasa Wachoma Nyama wa Jijini Mwanza

KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager jana imetoa mafunzo kwa wachoma nyama kutoka Baa mbali mbali za Mkoa wa Mwanza ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2014 yatakayo fanyika katika viwanja vya Furahisha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Ziwa, Erick Mwayela, alisema lengo la kutoa mafunzo ni kutoa elimu kwa wachoma nyama ukizingatia uchomaji nyama ni moja sehemu ya kujiingizia kipato katika Bar.

Kwa upande wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Laurence Salvi ambaye pia ni Jaji Mkuu wa mashindano hayo amesema huwezi kuandaa mashindano bila ya kutoa Elimu, hivyo TBL wamefikiria jambo la msingi sana lenye manufaa kwa waandaaji yaani wachoma nyama mpaka kwa watumiani yaani mlaji.

Bwana Lawrence binfsi aliishukuru TBL kupitia bia ya Safari Lager kufikiria jambo zuri la kufadhili elimu kwa kwa wachoma nyama jambo ambalo si faida kwa wachoma nyama tu bali hata watumiaji sasa watakula nyama inayostahili.
Jaji Mkuu wa Safari Lager Nyama Choma, Lawrence Salvi, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Semina ya Wachoma Nyama Mkoa wa Mwanza ikiwa ni maandalizi ya Mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2014.
Baadhi ya wachoma Nyama Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Mkufunzina Jaji Mkuu wa Mashindano ya Safari Nyama Choma Mkoa wa Mwanza, Lawrence Salvi (hayupo pichani) ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama Choma.
Mmoja ya washiriki wa Semina ya Wachoma nyama Mkoa wa Mwanza akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad