HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 10, 2013

mashujaa band yashukuru vyombo vya habari na wadau wa muziki wa dansi kwa kuwawezesha kupata tuzo tano

UONGOZI wa Bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa 'Wana kibega', umewashukuru wapenzi, mashabiki na vyombo vya habari kuiwezesha bendi hiyo kuchukua tuzo tano za Kili Music Award 2013.

Bendi hiyo imefanikiwa kutwaa tuzo hizo mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo utoaji wa tuzo hizo ulifanyika Mliman City Dar es Salaam.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter, alisema kuwa ni jambo la kumshukuru Mungu na kila mdau wa muziki kwa kuweza kutupigia kura na kupata tuzo hizo.

Alisema kuwa kwa namna moja au nyingine bila ya kupata ushirikiano wao wasingeweza kufika hapo. Alisema kuwa kupata kwao kura nyingi zilizoiwezesha bendi yao kufika hapo ni kutokana na kupata ushikiriano mzuri toka kwa vyombo vya habari.

Sospeter alisema kuwa hivyo wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika albam yao ijayo, ambayo utambulisho wa nyimbo tatu utafanyika mara baada ya kumalizika kwa mwezi mtufu wa ramadhani.

"Tunashukuru sana kwa kutupa ushirikiano mzuri kwa kuweza kupata kura nyingi zilizoweza kutupa tuzo tano,"alisema Sospeter.
Rais wa bendi hiyo,Charles Gabriel maarufu kwa jina la Chalz Baba alisema kuwa tuzo hizo yeye pamoja na bendi yake wamepata nguvu mpya ya kufanya kazi zaidi na kujituma na kuahidi kuwa albamu yao mpya itakuwa kali ikiwa na lengo la kutoa shukrani ya kukubalika kwao kwa Watanzania.

"Nitumie nafasi hii kutoa pongezi kwa kila mmoja, ni vigumu kukutana na watu wote kuwashukuru lakini kwa kutumia fursa hii naamini wengi watafahamu namna ambavyo tunatambua mchango wao wa sisi kufika hapa.Usiku wa Kill Music Award mwaka huu umeandika historia kubwa katika bendi yetu,"alisema.

Rapa maarufu wa bendi hiyo, John Saulo a.k.a Furgeson, alisema kuwa ni furaha kwake na familia ya mashujaa bendi, kwa kuweza kuthibisha kile wanachokifanya, hivyo anapenda kutoa shukrani kwa wote waliosababisha wafike hapo.

Aliongeza kuwa anatambua namna bendi yao ambavyo inakubalika hata pale ambapo wanafanya onesho sehemu lakini kitendo cha mashabiki, wapenzi na v yombo vya habari katika jitihada zao imesaidia wapewe tuzo hizo.

"Tuzo hizi zimefungua ukurasa mpya kwetu, lakini pia imepunguza maswali kwa baadhi ya wale ambao waliokuwa wanatubeza na kutuona kama hatuna tunachokifanya,"alisisitiza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad