HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 28, 2011

MBEYA NDIO MABINGWA WAPYA WA KILI TAIFA CUP 2011

Nahodha wa timu ya Mkoa wa Mbeya,Ivo Mapunda akiwa ameshika kombe la ubingwa wa Kili Taifa Cup 2011 baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mh. Kassim Majaliwa leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid,Arusha.
Naibu Waziri wa TAMISEMI,Mh. Kassim Majaliwa, akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Michuano ya Kill Taifa Cap mwaka 2011, Kaptani wa timu ya mkoa wa Mbeya, Ivo Mapunda baada ya timu ya mkoa huo kuibuka washindi baada ya kuifunga timu ya mkoa wa Mwanza goli 1-0 wakati wa mchezo wa fainali uliofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Wachezaji na viongozi wa timu ya Mkoa wa Mbeya wakiwa na Kombe la Ubingwa
Wachezaji wakiwa na Kikombe na mfano wa hundi wa Sh Milion 40 walizokabidhiwa baada ya kukabidhiwa.

Na Mwandishi Wetu,Arusha.

TIMU ya Mkoa wa Mbeya (Mapinduzi Stars) imenyakuwa ubingwa wa michuano ya Kili Taifa Cup baada ya kuifunga Mwanza goli 1-0 katika mchezo wa hatua ya Fainali uliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo mjini hapa leo.

Dakika ya 88 ya mchezo,Mshambuliaji wa timu ya Mkoa wa Mbeya,Gaudence Mwaikimba aliwanyayua mashabiki wa soka na wapenzi wa Mbeya baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa krosi iliyochongwa na mchezaji mwenzie,Mwagane Yeya na kujaa wavuni.

Mbeya imejinyakulia kitita cha sh.milioni 40, huku washindi wa Pili timu ya Mwanza wakiondoka na sh.milioni 20 na mshindi wa tatu Ilala ikiibuka na sh.milioni 10.

Katika mashindano ya timu, Timu ya Ilala imeibuka na zawadi ya timu bora yenye nidhamu na sh.milioni 2.5, wakati mchezaji Bora ni Juma Mpola wa Mbeya ambaye amepata kitita cha sh.milioni 2.5, mfungaji bora ni Gaudence Mwaikimba alimejinyakuwa kitita cha sh.milioni 2 baada ya kufunga magoli 8.

Mwamuzi Bora ni Israel Nkongo aliyepata kitita cha sh.milioni 2, kipa bora ni Abdul Juma wa timu ya Ilala aliyejinyakulia kitita cha sh.milioni 2 na Kocha Bora ni Juma Mwambusi wa timu ya Mkoa wa Mbeya ambaye nae amejipatia kitita cha Sh.milioni 2.

Mgeni rasmi aliyekabidhi zawadi hizo alikuwa ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI,Kassim Majaliwa.

Mashindano haya yamedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager na masuala ya habari kuratibiwa na Kampuni ya Executive Solutions.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad