HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 20, 2011

KUMBUKUMBU



Marehemu Elizabeth A. Mwingira wakati wa uhai wake.

Ni masaa,siku,wiki na hatimae leo umetimiza siku arobaini tangu ulipotutoka mapema mwezi uliopita.Unakumbukwa na Mume wako Alphonce V. Mwingira na watoto wako Vitus, John na Honest tulikupenda sana.

Hata hivyo aliyekupa uhai na kukufanya Mke wa Alphonce na mama ya Vitus, John na Honest alikupenda zaidi. Katika kipindi cha uhai wako umefanya kazi kubwa sana hapa duniani ikilinganishwa na umri wako. Baadhi ya kazi hizo ni kusaidia na kuwezesha wasio na uwezo, kazi ya kuunganisha watu pale palipotokea matatizo, kazi za kijumuiya, na kadhalika.

Ulikuwa mcha Mungu usiyochoka. Sisi hatuna shaka yoyote kwamba sasa unapumzika kwa amani mbinguni. Tutakukumbuka milele.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana litukuzwe.

Alphonce

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad