HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 30, 2011

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU WAPYA LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Charles Amos , kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete, akimwapisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Eng. Mussa Ibrahim kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Hab Mkwizu, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimkabidhi zana za kazi Ndg. John Thomas Mngodo kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Anna Maembe. kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Sihaba Nkinga, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akimpongeza Mwamini Juma Malemi, aliyekuwa msaidizi wa Makamu wa Rais (Maendeleo ya Jamii na Kero za Wananchi) katika Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akifurahia na mtoto, Irene Simba ambaye ni mtoto wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Juma Malemi (kushoto) wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo.Picha na Muhidin Sufiani wa Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad