HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 5, 2010

viingilio mechi ya stars na morocco sasa ni mpango mzima

Kikosi cha Taifa Stars
Kikosi cha Morocco

Na Mwandishi Wetu.

BAADA ya kula za uso kwenye mechi ya Stars na Brazil, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeshika adabu na kupunguza vingilio vyake vya mchezo wa Stars na Moroco utakaochezwa Jumamosi ijayo kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2012 nchini Gunea.

Viingilo viivyotangazwa katika mpambano wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika(AFCON) ni pamoja na kile cha Sh 5,000 ambacho ni cha chini kabisa wakati kile cha juu ni Sh30,000.

Kutangazwa kwa viingilio hivyo vinavyoonekana kuwa nafuu kwa wapenzi wengi wa soka nchini ni kutimia kwa ahadi aliyoitoa juzi jijini Dar es Salaam Raisi wa TFF Leodegar Tenga wakati wa uzinduzi wa kampeni za kuishangilia Taifa Stars aliposema wamepanga kutoa unafuu ili wananchi wengi waweze kujitokeza.

Akitangaza viingilio hivyo,Afisa habari wa TFF Frolian Kaijage alisema kuwa kiingilio cha Sh 5,000 ni kwa wale watakaokaa jukwaa la kijani wakati kile cha Sh 30,000 ni kwaajili ya jukwaa maalum (VIP A).

Kaijage alivitaja viingilio vingine kuwa ni Sh 7,000 kwa Jukwaa la Rangi ya Bluu,Sh10,000 kwa jukwaa la rangi ya machungwa wakati VIP C kiingilio kitakuwa Sh 15,000 na Sh 20,000 kwa jukwaa la VIP B.

Alisema kuwa tiketi kwaajili ya mpambano huo zitaanza kuuzwa kesho baada ya kumalizika kwa uhakiki utakaofanywa leo baina ya shirikisho hilo,Polisi na Usalama wa Taifa.

Katika hatua nyingine Kaijage alisema kuwa waamuzi wa mpambano ambao wote wanatoka Mauritius wanatarajia kuwasili nchini kesho sambamba na kamisaa wa mchezo anayetoka Kenya.

Aliwataja kuwa ni Sochurn Raji atakayekuwa mwamuzi wa kati wakati Bootun Balkrishina na Bally Vivian wakiwa ni wasaidizi na kamishaa Muhammad Imterazi.

Katika hatuna nyingine Kaijage alisema kuwa msafara wa Morocco wenye jumla ya watu 40 unaojumlisha wachezaji na viongozi wa timu hiyo kutua nchini leo usiku saa 4.30 tayari kwa mchezo dhidi ya Stars.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad