HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 6, 2010

StarTimes yapunguza gharama za ving'amuzi vyao

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya StarTimes Charles Liu(kushoto) akionyesha mitambo inayotumiwa na kampuni hiyo kurusha matangazo kwa njia ya dijitali ili kuwawezesha wananchi wengi kuachana na teknolojia ya kale ya analogia. Kushoto ni Afisa Masoko Davis Mwijage.

NA ZAHRA MAJID-MAELEZO

Kampuni inayotamba kwa ving’amuzi vya bei rahisi na iliyosambaa ulimwenguni na Africa kwa ujumla (Star Times) imezindua tamasha la uuzaji wa ving’amuzi vyake leo jijini Dar-es-salaam sambamba na kutangaza kuwa wameongeza channel zaidi kukidhi haja ya watanzania.

Akizindua tamasha hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo bwana Charles Liu amesema kampuni yao imesambaa kwenye nchi 9 za Africa zikiwema Tanzania, Uganda, Rwanda, Guinea, Cote de voire na nyinginezo .

Tamasha hilo limeambatana na punguzo la bei kwa 14% kwa king’amuzi kija na pia punguzo kubwa kwa television za kisasa ambazo zimeunganishwa moja kwa moja na king’amuzi hicho.

‘Tumetoa punguzo kubwa la bei ndani ya mwezi huu wa kumi na pia tumeongeza chanel za E-star na Real ambazo zinaonesha burudani mbalimbali ikiwemo filamu kutoka Nigeria na sehemu nyingine” Aliongeza Liu.

Mbali na hayo pia kampuni hiyo imepanua huduma zake katika mikoa mingi ya Tanzania ambapo vituo vimefunguliwa Dodoma, Mwanza,Arusha , Mbeya na Moshi pia kuepusha usumbufu kwa wateja, wameamua kuuza vocha zake za kulipia bili ya mwezikatika maduka madogo yatakayopatokana kila sehemu.

Bwana Liu alizitaja baadhi ya chanel zinazopatikana kuwa ni MSNBC,Nood Tv,Fashion Tv, Discovery world,Nickeledeon kwa ajili ya watoto, MTV base, ANIMAX, Kidsco na nyingine nyingi. Pia wameanzisha utaratibu wa kutoa huduma kwa wateja kwa njia ya simu kwa masaa 24.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad