
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini pamoja na Rais wa Fifa,Sepp Blatta wakiwa na mabingwa wapya wa Dunia mara baada ya kuwakabidhi kikombe chao cha ubingwa walioupata kwa kuitungua timu ya Taifa ya Uholanzi bao 1-0 lililofungwa na mchezaji Andres Iniesta dakika nne tu kabla ya mechi kumalizika.utabiri wa Pweza umefanya kazi yake kama inavyopaswa.

Streika wa ukweli Duniani Kote,Ferdinando Torres akifurahia ubigwa uliotwaliwa na timu yake ya Taifa huko nchini Afrika Kusini leo.

Mfungaji wa goli pekee lililoipa ubingwa timu ya Taifa ya Hispania,Andres Iniesta akishangilia goli lake hilo huku akiwa ametoa jezi yake na kubaki na fulana ya ndani iliyokuwa na maandishi ambayo sikuweza kuyaelewa maana yake.sasa sijui yanasema kwama heko Pweza kwa utabiri wako wa ukweliiii???Hispania ndio mabingwa wapya wa kombe la Dunia kwa sasa.
Mkuu hiyo jezi inamaneno ya kumkumbuka mchezaji mwenzao wa timu ya Taifa lao, aliyekufa ghafla wakati akicheza mpira mechi ikiendelea...aliangukaga ghafla na kupoteza uhai wake kiwanjani, miaka kama sikosei mitatu iliyopita. Sasa Iniesta kamwenzi na kumshirikisha ukindi huo kwa kumkumbuka kwa maneno mazuri haya kwa Kispansh; marehemu huyo alikuwa akiitwa Jarque, anasema; Jarque upo nasi daima!
ReplyDeleteCHIBIRITI.