
Mume wa Marehemu Primitiva Pancras ambaye alikuwa mwandishi wa habari wa kampuni ya New Habari Cooparation 2006 Bw. Joachim Mushi akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya mke wake yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam,
Marehemu Primitiva alifariki juzi mkatika Hospitali ya Lugalo baada ya kuugua ghafla na kupoteza uhai wake,Marehemu atakumbukwa kwa uwezo wake wa kuandika habari na makala zenye mguso kwa jamii hivyo kujipatia heshima kubwa kwa wasomaji wake ingawa alikuwa bado mchanga kwa kiasi fulani katika fani hii ya uandishi.

Waombolezaji wakibeba Jeneza lililowekwa mwili wa Marehemu Primitiva Pancras tayari kwa mazishi katika makaburi ya Kionodoni leo.

Bw. Joachim Mushi ambaye ni Mhariri wa makala wa Gazeti la Jambo Leo akiuaga mwili wa marehemu mke wake Primitiva Pancras kwa majonzi makubwa wakati wa ibada ya kuaga mwili huo iliyofanyika kwenye kanisa katoliki la Hananasifu Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Primitiva Pancars AMEN.
No comments:
Post a Comment