HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 13, 2010

tanzania mitindo house yazindua rasmi kituo cha kuchezea watoto-kigamboni

Mwenyekiti wa kituo cha Tanzania Mitindo House,Khadija Mwanamboka akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.Khadija alisema kuwa kituo hicho kimetengenezwa kwa msaada wa makampuni ya Bench Mark Productios,RBP OIL& Industrial Technology Ltd pamoja na Urban Pulse,ambacho kimegharimu shilingi za Kitanzania Milioni sita na laki saba.Udhamini wa ufunguzi wa kituo hicho umedhaminiwa na Kiondo Commonications International na Digital Art.Khadija aliongeza kuwa atahakikisha watoto Yatima wanapata fursa ya kucheza kama watoto wenye Wazazi na watajitahidi kuboresha kituo hicho kwa kuweka jukwaa la kuimba na kucheza pamoja na vifaa vya michezo vya watoto.Rais wa kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos,akishukuru kwa nafasi aliopewa ya uzinduzi wa kituo cha kuchezea watoto kilichopo huko Kigamboni. picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad