HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 15, 2010

Rais Kikwete Afungua Hotel Ya Lake Tanganyika Mkoani Kigoma Leo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi hoteli ya Lake Tanganyika mjini Kigoma leo mchana.Kushoto ni Mmiliki wa hoteli hiyo Bwana George Nzunda na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Simbakalia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Hoteli ya Lake Tanganyika mjini Kigoma muda mfupi baada ya kuifungua leo mchana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe muda mfupi baada ya kuwasili mjini Kigoma leo mchana tayari kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Simbakalia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mandhari ya Hoteli ya Lake Tanganyika muda mfupi baada ya kuifungua mjini Kigoma leo mchana.Kulia ni Mmiliki wa Hoteli hiyo Bwana George Nzunda na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa kigoma Kanali Simbakalia.

Rais Jakaya mrisho Kikwete akisalimiana na mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Baadhi ya wakazi wa kigoma wakimlaki Rais kikwete kwa ngoma za utamaduni baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma kwa zaiara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.
(picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad