HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 4, 2010

EXCLUSIVE INTERVIEW YA JUSSA

MO Blog: Kuna mpasuko mkubwa baina ya watu wa visiwani kutokana na tofauti ya itikadi za kisiasa, sasa wewe unafikiri ni njia gani zinaweza kuziweka pande mbili hizo pamoja wasahau tofauti na wajenge nchi ili visiwa vya Zanzibar vifike mbali kimaendeleo?

JUSSA: Kuna mjadala mpaka leo iwapo kweli mpasuko upo au la. Wapo wanaokubali upo wengine wanaukataa, lakini mimi ningependa niweke wazi kwamba kwa mawazo yangu mgawanyiko uliokuwepo sio mgawanyiko wa visiwa na pia sio mgawanyiko wa watu bali ni mgawanyiko wa wafuasi wa vyama vikuu vya siasa.

Na nina utazama mgawanyiko huo katika sura mbili, wa kwanza ni mgawanyiko uliosababishwa na matukio ya kihistoria, na pili umesababishwa na kutokuwepo na uwiano wa kufanya shughuli za kisiasa.

Kwa upande wa historia, Zanzibar imepita kwenye vipindi vingi vya kihistoria. Ni bahati mbaya kwamba kumekuwepo na majaribio ya ama kuifuta au kuipotosha historia hiyo. Upande mmoja hasa ule unaotawala unataka kuzungumzia Zanzibar mara zote katika enzi za za utumwa, na unataka ionekane kama vile ilikuwa biashara ya Waarabu dhidi ya Waafrika na hivyo kujaribu kuuonyesha mgogoro huu kuwa ni kama vita baina ya jamii moja na jamii nyingine. Hawa tatizo lao ni kuwa wanajaribu kukataa ukweli wa historia. Hakuna mtu anayeweza kukataa kuwa Zanzibar kulikuwa na utumwa, lakini ilikuwa sio Zanzibar peke yake nyakati hizo iliyokuwa na biashara hiyo bali nchi nyingi duniani, mfumo wa wakati huo ulikuwa wa mwenye nguvu kumshinda asiye na nguvu, haikuwa jamii fulani au kabila fulani dhidi ya jamii nyingine. Mimi mara zote hujiuliza kwa nini biashara ya utumwa ya magharibi mwa Afrika inaitwa Atlantic Slave Trade lakini ya huku inageuzwa kuwa Arab Slave Trade wakati sio Waarabu pekee waliokuwa wanunuzi wa watumwa na sio pekee waliohusika kwenye biashara hiyo. Ukitizama hata huku hao watumwa wengi walikuwa wakitoka Bara, na watumwa waliouzwa ni matunda ya vita baina ya jamii za Kiafrika huku jamii iliyoshinda ikiwauza mateka wake kwenye biashara hiyo hivyo Machifu wa Waafrika na Waafrika wenyewe pia walihusika kwenye biashara hiyo.

Kwa mahojiano kamili www.mohammeddewji.com/blog

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad