HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 22, 2010

TBL Yazipatia Viatu Timu Nane Zilizoingia Robo Fainali katika Mashindano Ya Kili Taifa Cup


Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akimkabidhi viatu kocha wa timu ya Ilala,Jamhuri Kiwelu "Julio" kwa ajili ya timu yake hiyo iliyoingia katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya Kili Taifa Cup yatakayoanza kutimua vumbi katika hatua hiyo ya robo fainali ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akikabidhi viatu kwa Ramadhan Mahano ambaye ni Katibu Msaidizi wa IRFA,kwa ajili ya timu ya Iringa.
Muwakilishi toka Timu ya Mwanza,Ngawina Ngawina nae akipoke viatu kwa niaba ya timu yake toka kwa Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George kavishe katika hafla fupi iliyofanyika leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF,Ilala
Katibu wa Chama cha Soka cha Temeke,Bakili Makele akipokea viatu vitakavyotumika katika michezo ya hatua ya robo fainali katika mashindano ya kili Taifa Cup,toka kwa Meneje wa bia ya Kilimanjaro,George Kavishe,makabidhiano hayo yamefanyika leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za TFF,Ilala.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad