leo nimepata heshima kubwa sana ya kukutana na mkongwe wa muziki wa rumba anaefanya shughuli zake hizo za muziki nchini Sweden anaefahamika kwa jina la Dekula Kuhanga ambaye kwa sasa yuko hapa nchini kwa mapumziko mafupi na baadae atarejea nchini Sweden anakoendeleza libeneke lake la muziki.Kuhanga ambaye ni mkongwe wa muziki wa rumba hapa nchini na ni mmoja kati ya wanamuziki waanzilishi wa Bendi ya Maquis iliyokuwa ikifanya vyema sana miaka ya nyuma yeye akiwa ni mpiga mpini na muimbaji na pia ni mtunzi wa nyimbo,amenitonya kuwa sasa hivi yeye anamiliki bendi yake huko nchini Sweden na yuko mbioni kuachia bonge moja la albam ambalo hakutaka kuwa wazi kwamba litakuwa na nyimbo ngapi na kuendelea kutoa ahadi kwamba wasabiki wake wavute subira kuisikilizia albam hiyo ambayo imebeba jina la GOD IS ONE ambayo tayari keshaiachia na Video yake (icheki hapo Chini).anasema hiyo ni kama trela tu sasa msubiri picha yenyewe ambayo si muda mrefu itaanza kuwa mitaani baada ya kuikamilisha.
Hebu Cheki Kideo Hiki Halafu Utapata Jibu Kwamba Hiyo Albam Itakuwa Ni Ya Namna Gani.
WEKA HII KULE KWA KAKA MICHUZI HII INANIKUMBUSHA KINA KING KIKII NA HAMZA KALALA HII NDIO FULL SOUND YA TANZANIA SIO TWANGA PEPETA AU BONGO FLAVA KAZI NZURI SANA HII KAMA TUNE ZA SOUND BEAT NA KINANDA TUTARUDISHA HIVYO BASI MUZIKI WETU UTAJULIKANA KWA AWARD ZITAPATIKANA.
Huyu mjomba ni kati ya wachache saana waliobakia na kulichalanga gitaa kitaalamu,akipagawa huwa analipaga kwa kutumia ulimi,big up saana Vumbi!endeleza Rumba mkuu tunakutegemea,na huko bongo kula bata,na usisahau kutunga nyimbo kulingana na mazingira na maisha unayoyashuhudia ukiwa huko likizoni
WEKA HII KULE KWA KAKA MICHUZI HII INANIKUMBUSHA KINA KING KIKII NA HAMZA KALALA HII NDIO FULL SOUND YA TANZANIA SIO TWANGA PEPETA AU BONGO FLAVA KAZI NZURI SANA HII KAMA TUNE ZA SOUND BEAT NA KINANDA TUTARUDISHA HIVYO BASI MUZIKI WETU UTAJULIKANA KWA AWARD ZITAPATIKANA.
ReplyDeleteHuyu mjomba ni kati ya wachache saana waliobakia na kulichalanga gitaa kitaalamu,akipagawa huwa analipaga kwa kutumia ulimi,big up saana Vumbi!endeleza Rumba mkuu tunakutegemea,na huko bongo kula bata,na usisahau kutunga nyimbo kulingana na mazingira na maisha unayoyashuhudia ukiwa huko likizoni
ReplyDelete