HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 18, 2010

ARV'S Zazuia Maambukizi ya HIV

Habari hii kutoka BBC imeniacha nikiwa nakuna kichwa kwa sababu bado iko na mapungufu mengi, naomba uisome na wewe halafu tuelekezane kama kichwa changu ndio kigumu kuelewa au na wewe umebaki mdomo wazi kama mimi.

Mtandao wa shirika la habari la BBC unatuhabarisha kwamba, "Utafiti mpya umeonyesha kuwa dawa zinazotumika kutibu maradhii tegemezi kwa wagonjwa wa ukimwi (ARVS) zinaweza kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV.

Utafiti uliofanywa miongoni mwa wanandoa elfu tatu mia tano wanaogua virusi hivyo barani afrika , ulionyesha kuwa uwezekano wa wagonjwa waliotumia sana dawa za ARV,'s kuwaambukiza wenzao, ni wa chini mno.

Kwa kipindi cha miaka mitatu, zaidi ya visa mia moja vya maambukizi mapya ya HIV viliripotiwa miongozi mwa waliokuwa wanafanyiwa utafiti huo. Lakini ni mtu mmoja tu aliyekuwa anatumia dawa hizo ndiye alieambukizwa.

Waliofanya utafiti huo, wanasema huenda mtu huyo aliambukizwa kutokana mabadiliko mwilini mwake yaliosababishwa na dawa hizo."

Tatizo langu ni kwamba napata shida kuiamini habari hii kwa sababu hatuambiwi waziwazi
1) ni shirika gani hasa limefanya utafiti huu

2) Je watafiti wana uhakika gani kwamba wanandoa hao mbali na kutumia dawa walikuwa pia hawatumii kondomu wakati wa kujamiiana?

3) Ni mabadiliko gani yaliyofanya huyo mtu mmoja kuambukizwa VVU? Maana tunaambiwa kwamba huenda mabadiliko mwilini ndiyo yaliyopelekea mlengwa mmojawapo kupata maambukizi.

Naliheshimu sana shirika la habari la BBC, lakini hadi hofu zangu tatu nilizoorodhesha hapo juu zitakapowekwa sawa ndio roho yangu itatulia. Ila kama habari hii ni ya kweli bado nakushauri mdau njia ya uhakika zaidi ya kuepuka maambukizi ni kuepuka ngono zembe na kutumia kondomu ukishindwa kabisa.

1 comment:

  1. Sasa kaka wewe huoni kuwa jamaa wamesema kuwa "zinaweza kuzuia" hawajafanya conclusion yeyote kwenye hili.

    Kuhusu reseach siyo lazima shirika fulani wafanye utafiti, inaweza kuwa ni kitengo fulani kama Chuo, au group la wataalamu wanafanya utafiti kwa janga hili la Ukimwi.

    Swali lako la pili ndilo limeniacha nacheka, unajua kama unafanya utafiti lazima uwe na kazi wataalam wanasema samples. Kumbe kuna njia mbalimbali za kufanya utatifiti, inaweza kucha random, selective and etc. Kwa utafiti huu kwa ujumla wamefanya selective, yaani wamechangua namba ya sample...yaani hawa watu wenye Virus ndipo wakafanya utafiti wao na wakaja na matokeo hayo.

    Nilipenda kujibu swali lako kwa ufupi.

    Alex

    ReplyDelete

Post Bottom Ad