HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 17, 2009

hukumu ya zombe na wenzie imeanza kusomwa mahakama kuu leo

Abdallah Zombe akiongea na wakili wake Mh. Jerome Msemwa


Hukumu ya kesi ya mauaji iliyohusisha askari wa Jeshi la Polisi 9 pamoja na aliyekuwa mkuu wa upelelezi Dar Abdallah Zombe imeshaanza kusomwa Mahakama Kuu na hivi tunavyoongea Jaji Salum Masati yuko kwenye kusoma muhstasari wa hatua ya kesi hiyo ambapo sasa yupo kipengele cha shahidi wa 34.

Katika kesi hiyo ilipoanza rasmi kusikilizwa Mei 28, 2008, Zombe na wenzake wanatuhumiwa kuwaua kwa kukusudia Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi na Mathias Lunkombe ambao walikuwa wafanyabiashara wa Mahenge, pamoja na dereva teksi wa Manzese jijini Dar es salaam, Juma Ndugu.

Inadaiwa kuwa watu hao waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye msitu wa Pande ulioko Mbezi Luisi wilayani Kinondoni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Watu hao walikamatwa na polisi kwa madai ya kuhusika kwenye tukio la ujambazi jijini Dar es salaam, ikaja kushukiwa kuwa waliouawa hawakuwa majambazi taarifa ambayo JK aliunda tume chini ya Jaji Kipenka Mussa ambayo uchunguzi wake ulisababisha kutiwa hatiani kwa watu hao na kufunguliwa kesi.taarifa hii ni kwa hisani ya mzee wa libeneke ambaye yupo eneo la tukio kutupatia kila kinachojiri huko Mahakama kuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad