HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 15, 2009

wakuu 11 wa mikoa wabadilishwa vituo vya kazi

RAIS Jakaya Kikwete amebadilisha vituo vya kazi kwa Wakuu wa mikoa 11 ambapo mkuu wa mkoa wa Dodoma William Lukuvi atakuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam na Abbas Kandoro anakwenda Mwanza.
Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa imesainiwa na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri, lengo la mabadiliko hayo ni kutoa msukumo zaidi wa shughuli za serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. James Msekela anahamia Dodoma.Wakuu wa mikoa wengine waliobadilishwa ni Enos Mfuru kutoka Kagera kwenda Mara, Issa Machibya kutoka Mara kwenda Morogoro, Said Kalembo kutoka Morogoro kwenda Tanga, Mohamed Abdulaziz kutoka Tanga kwenda Iringa na Amina Mrisho kutoka Iringa kwenda Pwani.
Wengine ni Dk. Christine Ishengoma kutoka Pwani kwenda Ruvuma, Monica Mbega kutoka Ruvuma kwenda Kilimanjaro na Mohamed Babu kutoka Kilimanjaro kwenda Kagera.
Mabadiliko hayo ya wakuu wa mikoa yamefanyika wiki tatu tangu Rais Kikwete afanye uteuzi wa wakuu wa wilaya kwa kuteua wapya 15

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad