HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 12, 2008

Zain Yajiwa Juu Na Basata Kuhusiana Na Ujio Wa Kikundi Cha Umoja

BARAZA la Sanaa la Taifa(BASATA)kupitia kamati ya vibali imewapa muda wa siku nne Kampuni ya simu ya mkononi ya Zain kujieleza kutokana na kudaiwa kuingiza nchini kundi la Umoja Group(Pichani)toka Afrika Kusini bila kibali cha Baraza.
Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa kwenda kwenye kampuni hiyo kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa baraza hilo Bw.Lauwo ilisema Kamati ya Vibali vya Wasanii imebaini kuwa kampuni ya Zain ilileta kikundi cha Umoja Group toka afrika Kusini bila kibali cha baraza.
Alisema kikundi hicho kilifanya onyesho katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Kampuni hiyo bila kibali cha Kamati ya Taifa ya Vibali vya wasanii ambayo ndiyo yenye dhamana ya kutoa vibali vya wasanii wanaoingia nchini Lauwo alisema kutokana na hali hiyo Kamati ya Vibali inaipa nafasi ya kutoa maelezo kwa maandishi kwa nini Kampuni hiyo isichukuliwe hatua za kisheria kwa uvunjaji huo wa makusudi kwa kuipa muda hadi Agosti 14,mwaka huu kuwa imepeleka maelezo katika baraza hilo.
Alisema kampuni ya Zain ilifanya hivyo wakati ikijua haina mamlaka wala haijasajiliwa kuingiza nchini vikundi vya sanaa na kufanya maonyesho huku mila,desturi na sanaa za nchi ya Afrika Kusini na Tanzania zinatofautiana na kampuni hiyo kwa makusudi ikaleta kikundi kilichocheza jukwaani wakiwa maungo ya miili yao nje.
Alisisitiza kuwa pia kampuni hiyo bila kufuata taratibu za uingizaji vikundi nchini,ilikusudia kuinyima serikali mapato yake halali kutokana na maonyesho yao na na kulenga kuwadhalilisha watanzania walioona aonyesho hayo na wasanii hao kwa kuvaa nusu uchi.

1 comment:

Post Bottom Ad