
Wafanyakazi wa Kampuni ya Pure Natural Baby Diapers wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Pure Natural Baby Diapers imesisitiza dhamira yake ya kulinda afya ya watoto wachanga na kuhifadhi mazingira baada ya kutembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya pampasi kwa watoto Wachanga.
Elimu hiyo iliyotolewa katika wodi ya wazazi imelenga kuwasaidia wazazi na walezi kuelewa umuhimu wa kuchagua pampasi salama tangu siku za mwanzo za maisha ya mtoto, huku wakijifunza namna uchaguzi huo unavyoweza kumkinga dhidi ya maambukizi na matatizo ya ngozi.
Akizungumza katika tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam Februari 5, 2026 jijini Dar es Salaam hilo, Mwakilishi wa Masoko wa kampuni hiyo, Stumai Kiwanga, amesema pampasi za Pure Natural zimebuniwa kwa kuacha wazi eneo la kitovu ili kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa.
“Ubunifu huu unasaidia kitovu kukauka haraka na kupunguza hatari ya maambukizi kwa mtoto mchanga,” amesema.
Ameongeza kuwa pampasi hizo zina uwezo mkubwa wa kunyonya unyevunyevu, hivyo kusaidia ngozi kubaki kavu kwa muda mrefu.
“Ngozi kavu humlinda mtoto dhidi ya muwasho na vipele. Tunataka mtoto awe salama na mwenye faraja katika mazingira bora kiafya,” amefafanua.
Mbali na afya ya mtoto, kampuni hiyo imezingatia uhifadhi wa mazingira kwa kutumia malighafi zinazotokana na mimea.
“Teknolojia hii rafiki kwa mazingira inalenga kupunguza taka ngumu na kulinda mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Afya ya mtoto na afya ya dunia vinaenda pamoja,” amasema Stumai.
Kuhusu matumizi, ameeleza kuwa pampasi hizo zina mfumo wa kuonesha ishara zinapokuwa zimejaa ili kumwezesha mzazi kubaini muda sahihi wa kumbadilisha mtoto.
“Hii husaidia kumhudumia mtoto kwa wakati na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya pampasi, hivyo kupunguza taka za kimazingira,” ameongeza.
Aidha, pampasi hizo zimetengenezwa bila kemikali hatarishi na zina upindo unaozuia kuvuja kwa unyevunyevu. “Usalama wa mtoto ndio kipaumbele chetu; ndiyo maana tumetengeneza pampasi laini na salama kwa ngozi nyororo ya mtoto mchanga,” amesisitiza.
Kwa upande wake, Neema Peter, mkazi wa Kigamboni aliyefika kujifungua Muhimbili, amesema pampasi hizo zitasaidia kuharakisha uponaji wa kitovu cha mtoto wake kutokana na hewa kupita kwa urahisi.
“Tunashukuru sana kwa kutupa msaada huu,” amesema, akipongeza kampuni hiyo kwa mchango wake kwa wazazi na watoto wachanga.
#Purefromthefirsttouch#campaign#


No comments:
Post a Comment