HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 8, 2025

HaloPesa Yazidi Kuwazawadia Wateja Kupitia Kampeni ya “Tamba na Bonasi”

HaloPesa Tamba na Bonasi imezidi kukiwasha zaidi katika soko la huduma za kifedha Tanzania, baada ya kufanikiwa kuwazawadia zaidi ya washindi 400 ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu kuzinduliwa kwake.

Kupitia kampeni hii, wateja wa HaloPesa wamekuwa wakipata nafasi ya kujishindia bonasi mbalimbali kila wanapofanya miamala, ikiwemo kutuma pesa, kutoa pesa, kulipa bili, au kulipia bidhaa kupitia HaloPesa.

Miongoni mwa washindi waliobahatika kujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja (1,000,000) kutoka kwa Mr Bonasi, Bw.Selemani Khalfan, ambaye amejishindia Bonasi ya shilingi Milioni 1, ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya kampeni hii inayolenga kuwazawadia wateja wanaotumia HaloPesa katika shughuli zao za kila siku.

Akizungumza wakati wa kuwapongeza washindi hao, Afisa Masoko wa HaloPesa, Bi. Aidat Lwiza, alieleza kuwa kampeni ya Tamba na Bonasi ni sehemu ya jitihada za HaloPesa kuwashukuru wateja wake kwa kuendelea kutumia huduma zao, sambamba na kuhamasisha matumizi ya teknolojia rahisi katika miamala ya kifedha na kutimiza miaka 9 Tangu kuanzishwa kwa HaloPesa.


“Kupitia HaloPesa, tumerahisisha maisha ya wateja wetu. Wateja wetu waendelee kufanya miamala kwa urahisi, haraka na unafuu, huku wakiendelea kujipatia nafasi ya ushindi hadi Milioni 2 kutoka kwa Mr. Bonasi kila siku, kila wiki na kila mwezi. 

Kila muamala ni nafasi ya ushindi, aliongezea kwa kusema Halotel na HaloPesa itawasiliana na Wateja wake kupitia namba 100 pekee!” alisema Bi. Aidat Lwiza Afisa Masoko HaloPesa.

“HaloPesa, Tumerahisisha kwa makato nafuu zaidi!”







No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad