Wednesday, June 4, 2025

DMI YATOA ELIMU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MAJINI JIJINI DODOMA


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
CHUO cha Bahari Dar es Salaam (DMI) yatoa elimu ya utunzaji wa mazingira majini wakati wa maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.

Akizungumza katika maonesho hayo Mkufunzi wa DMI, Nahodha Robert Mollel, amesema chuo kupitia programu zake kinawajengea wanafunzi uelewa na ujuzi wa kuzingatia viwango vya kimataifa vya usalama, uhifadhi wa mazingira ya baharini na matumizi sahihi ya teknolojia rafiki Kwa mazingira, hasa katika zama hizi za changamoto za plastiki na mabadiliko ya tabia nchi.

Kauli mbiu ya Siku ya Mazingira Duniani katika mwaka huu isemayo “Mazingira yetu na Tanzania ijayo, tuwajibike sasa; Dhibiti Matumizi ya Plastiki.”

Ni kauli inayotufundisha kuwa mustakabali wa taifa letu unategemea hatua tunazochukua leo katika kulinda na kuhifadhi mazingira.

DMI imeshirikiana na taasisi mbalimbali kufanya usafi katika uwanja wa ndege wa Dodoma na upandaji wa miti kwenye stesheni kuu Samia Suluhu Dodoma ” aliongeza.

Mollel alisisitiza kuwa “Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha tunalinda mazingira kwa ustawi wa vizazi vijavyo,”

Maonesho haya yameanza tarehe 1 Juni na kukamilika tarehe 5 Juni 2025.






Matukio  mbalimbali katika maadhimisho ya Siku ya mazingira duniani Mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment