HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 25, 2025

Bodi ya TASAC yataka matokeo ya tija katika ya uwekezaji wa Bandari

 

Wajumbe wa Bodi ya TASAC wakiangalia ujenzi wa maboresho ya Bandari ya Bukoba wakati walipofanya ziara katika  Bandari hiyo.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Bandari ya Bukoba
Bodi ya Wakurugenzi wa TASAC  ,Watumishi wa TASAC,TPA  wakiwa katika bandari  ya Kemondo

Baadhi picha katika Matukio  ya bodi ya TASAC katika Bandari ya Kemondo na Bukoba.

Na Mwandishi Wetu ,Bukoba

Bodi ya Wakurugenzi  wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi ya ujenzi wa Bandari za Kemondo na Bukoba hivyo fedha hizo zinatakiwa kuleta tija na zirudi kutokana huduma zitazotolewa na Bandari hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati ziara Bodi katika Bandari hizo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Nah.Mussa Mandia amesema kuwa baada ya maboresho ya miundombinu ya ujenzi wa bandari watahudumia mizigo na abiria kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa awali.

Amessema kuwa fedha ya Bandari ya Kemondo bilioni 20 na ujenzi wake umekamilika ambapo huduma zake zimeongezeka hadi kufikia tani 150000 kwa mwezi na mapato yake yameongezeka mara tatu huku Bandari ya Bukoba ujenzi wake ukiwa katika hatua za mwisho unaogharimu zaidi ya sh.Bilioni 19.

Amesema  kuwa kama wadhibiti ni kuhakikisha Bandari hizo zinaendelea kutoa huduma bora na tija kwa serikali huku akitaka wasimamizi wa bandari kusimamia kwa  weledi.

Amesema Serikali ya awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kutimiza ndoto katika upanuzi wa bandari za Kemondo na Bukoba ambayo miundombinu yake ilikuwa ya zamani ambapo haiendani na mahitaji ya sasa.

Hata hivyo amesema kazi bodi itaendelea kushauri katika taasisi wanayoidhibiti ambapo matokeo yake yanaonekana kwa miradi mbalimbali kwenye bandari nchi nzima

Mkuu wa  Bandari ya Bukoba wa TPA Malick Ismail amesema kuwa Bandari hiyo maboresho ya ujenzi bandari hiyo baada ya kukamilika watahudumia meli nne kwa wakati mmoja tofauti na ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wakihudumia meli moja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad