Umoja
wa wenye mabenki Tanzania (TBA) umezindua kampeni ya kuhamasisha elimu
ya Kifedha iitwayo Niko Fiti. Akizungumza wakati wa uzinduzi Naibu
Gavana wa Benki Kuu Dr.Bernard Kibese alizipongeza benki kwa kubuni
mkakati huu Na kuzitaka kuendelea kuongeza ubora wa huduma zao Na elimu
ya fedha kwa wateja.
Kwa upande wake mwenyekiti TBA Abdulmajid
Nsekela amesema Niko Fiti ni mkakati mahususi wa kuongeza elimu Na
kujali wateja unatekelezwa Na wanachama wote wa TBA. Tunafurahi pia
kwamba mkakati huu unakuja wakati wa wiki ya wateja inaanza hivyo kwenda
sambamba Na umuhimu wa kuboresha huduma Na uelewa wa wateja wa huduma
za kibenki.
No comments:
Post a Comment