
Na Mwandishi Wetu
KATIKA
kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) imetoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto kutembelea
makumbusho ya mawasiliano yanayoelezea maendeleo na ukuaji wa
teknolojia za mawasiliano duniani na hakuna gharama ya kuingia katika
Makumbusho hayo ni bure.
TCRA inaadhimisha wiki ya huduma kwa
wateja kwa kutoa wito kwa wazazi na shule pamoja na wananchi kwenda
katika makumbusho ya Mamlaka kujifunza vitu mbalimbali vilivyotumika
katika Mawasiliano kabla ya ukuaji wa Teknolojia ya Mawasiliano
haijaanza.
Katika Maadhimisho hayo Mamlaka imejenga dawati maalum la kuhudumia wateja kutokana na huduma wanazozitoa.
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mabel Masasi amesema
Maadhimisho hayo wanatarajia kupata maoni yao katika utoaji wa huduma
kwa Mamlaka na kuangalia kujipanga katika mikakati.
Amesema Maadhimisho hayo ya huduma kwa wateja hufanyika kwa mwaka mara moja hivyo ni fursa ya wadau kujitokeza na kutoa maoni
"Tunaendelea
kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja tukilenga kupata maoni yao na
kutembelea katika dawati maalum lililoanzishwa kwa ajili hiyo"amesema
Mabel.
Hata hivyo katika kuadhimisha Maadhimisho hayo kuna
mikakati mbalimbali imewekwa kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanapata
huduma Bora za Mawasiliano.


No comments:
Post a Comment