Thursday, December 13, 2018

NAIBU WAZIRI ULEGA AAGIZA WAVUVI WASAJILIWE KATIKA VIKUNDI

 NAIBU waziri wa mifugo na uvuvi Abdalla Ulega amewaagiza watendaji wa Halmashauri ya Kilombero  kuhakikisha wavuvi wote wanasajiliwa na kuwa na vikundi ndani ya mwezi mmoja ili waweze kufanya shughuli zao na kuchangia pato la taifa.

Ulega amewataka kuwaangalia wavuvi hao kama wanauhitaji wa kupata vitambulisho vya wajasiriamali alivyovitoa Rais John Magufuli wapewe ili wafanye kazi zao bila bugudha.

Akizungumza katika ziara aliyoifanya katika kijini cha Miwangani kata ya Idete wilayani humo na kutatua migogoro mbalimbali Ulega amesema kuwa wavuvi lazima wathaminiwe na kupatiwa haki zao hasa za kuwa na vikundi mbalimbali hivyo haina budi kufanya tathimini na kuwasajili ili waweze kutambulika kwani nao husaidia katika kuchangia pato la taifa.

Ulega amesema kuwa kabla ya mwezi Januari atatembelea na kuongea na wavuvi hao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kama maagizo hayo yametekelezwa vyema.

Kwa upande wao wavuvi na wafugaji wamempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake za kujenga Tanzania mpya na hasa kwa  kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini na wamemshukuru Waziri na Naibu waziri wa mifugo na uvuvi kwa ushirikiano wanaoutoa katika kukuza na kuimarisha sekta hiyo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji,wavuvi wa jijini cha  Miwangani wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro.ziara ya Kuzikiliza kero mbalimbali za wafungaji,wavuvi na kuzitatua.

Katibu Tawala wa wilaya ya Kilombero,Robert Sidasela akizungumza na wafugaji na wavuvi wa kijiji cha Miwangani wilaya ya Kilombero  kuhusu mipaka ya wakulima na wafungaji  iliyowekwa na  Serikali.

 Wananchi wa kijiji cha Miwangani akumshukuru Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega kwa kufika katika kijiji hicho na kuwatalulia kero zao na muda mrefu.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

 Sehemu ya Wananchi wa kijiji cha Miwangani wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro wakimsikiliza Naibu wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.




No comments:

Post a Comment