MENEJA
wa Bandari ya Tanga (TPA) Percival Salama kulia akimueleza Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage mipango ya bandari hiyo
na namna walivyoboresha huduma zao kwa wafanyabiashara wanayoitumia
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akisalimia na Meneja
wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya kuwasili kwenye
viwanja vya Mwahako Jijini Tanga alipokwenda kufungua maonyesho ya sita
ya biashara ya kimataifa
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kushoto akisisitiza
jambo kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya
kufungua maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye
viwanja vya Mwahako Jijini Tanga katikati ni Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martine Shigella
MENEJA
wa Bandari ya Tanga (TPA) Percival Salama amesema wanajivunia
kuboreshwa huduma zao kwa kiwango kikubwa ikiwemo uandaaji wa nyaraka
kwa kasi na usalama wa kutosha kwa wateja na hivyo kutumia muda mfupi
kutokana na taasisi zinazohusika kuwepo sehemu moja hivyo kuwawia rahisi
kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati mmoja.
Salama aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye
viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya kimataifa ya
sita ya biashara ambapo alisema kutokana na hali hiyo hakuna sehemu
ambayo mteja anaweza kupita akikwama bila wao kujua mara kila hatua
wanazokuwa wakipitia wanatambua mara moja.
Alisema kuwa sehemu ambazo mteja anaingia kwenye bandari hiyo anapata
taarifa moja kwa moja hiyo ikiwa wanakumbana na vikwazo vya namna yoyote
zikijitokeza inawawia rahisi kuweza kuona na kuvishughulia kwa muda
mfupi ili kuweza kuondoa usumbufu ambazo unaweza kuwakabili
wafanyabiashara.
“Kwa kweli huduma za bandari ya Tanga tumeziboresha kwa kiasi kikubwa
kutokana na kasi ya uandaaji wa nyaraka lakini hata usalama wa kutosha
kwa wateja ambao wamekuwa wakiitumia hali iliyofanya kutumia muda mfupi
kutokana na taasisi zinazohusika kuwepo sehemu moja hivyo kuwawia rahisi
kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati mmoja “Alisema.
Akizungumzia ujenzi wa gati,Meneja Salama alisema gati hilo litakalokuwa
la usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari
ya Tanga hakutakuwa na uchimbaji eneo hilo kwani lina kina zaidi ya
mita 20 linajisholeza na meli zinazotarajiwa kubeba tani laki moja hadi
laki mbili na nusu kuingia na kufanya upakuaji.
“Sehemu ambayo serikali na TPA inataka kuchimba eneo ambalo kuna gati ya
sasa kwa muda wa miaka 129 wanahudumia meli nangani kwani wanaona
msingi wake uwezo wa Bandari ya Tanga ni shehena 750,000 lakini mwaka
2016 Bandari hiyo ilizidi kiwango cha uhudumiaji na kufikia tani 843,000
hivyo kutokana na matokeo hayo wakaona ipo haja ya kuboresha Bandari
hii”Alisema.
Alisema mwaka Agosti 8 mwaka jana Rais Dkt John Magufuli akiwa mkoani
Tanga alitoa maagizo kuwa anataka bandari ya Tanga inayohudumia mizigo
sasa ichimbwe na meli zifike kwenye gati ambapo wao tayari wamekwisha
kuanza utekelezaji wa agizo hilo.
Meneja huyo alisema wameanza kutekeleza maagizo hayo tayari mkandarasi
wa BICO ameingia kazini na amesaini mkataba wa miezi minne kuanza
kufanya kazi ya utafiti kwenye eneo la sasa la Bandari ili kujua chini
ya bahari kuna udongo wa namna gani ili hatua nyengine ya kumpata
mkandarasi kwa ajili ya ujenzi na ushauri zifanyike.
No comments:
Post a Comment