HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 18, 2017

MKUTANO WA 20 WA SIKU YA BIMA WAFANYIKA MKOANI TANGA, WAUNGA MKONO UCHUMI VIWANDA

Wadau wa sekta ya bima nchini wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (aliyekaa wa tatu kulia) katika mkutano wa 20 wa siku ya bima nchini uliofanyika mwisho wa wiki jijini Tanga. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania.

TANGA: Taasisi ya Bima Tanzania imesherehekea mkutano wa 20 wa siku ya bima nchini kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali katika ufufuaji wa viwanda vya zamani nchini.

Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania, pia ulikutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya bima wa ndani na nje ya nchi, wizara mbalimbali na taasisi za umma na sekta binafsi mwishoni wa wiki jijini Tanga. Raisi wa Taasisi hiyo, Bosco Bugali alisema Taasisi hiyo inatambua umuhimu wa ujenzi wa viwanda vipya pamoja na ufufuaji wa viwanda vya zamani kwani viwanda huleta mabadiliko kiuchumi na maendeleo kwa binadamu.

“Mada kuu ya mwaka huu ni ‘Bima – Nguzo ya Viwanda’, mada hii inaonesha sera ya Serikali ya viwanda na inaonesha ahadi yetu kuelekea ajenda hii. Tunajiunga na Raisi wetu, Dk. John Pombe Magufuli ambaye alisisitiza mara kwa mara juu ya kukuza viwanda kwani viwanda huleta mbadiliko ya kiuchumi na maendeleo kwa binadamu”, alisema Bugali.

Aliongeza kuwa huduma za bima zinajumuisha jitahada ambazo serikali inafanya katika kukuza uchumi kwenda hatua nyingine. Nayo Serikali imeipongeza Taasisi ya Bima Tanzania kwa kuandaa mkutano huo na kutoa wito kwa makampuni ya bima yaliyopo nchini kutanua wigo wa huduma zake kwa kutoa huduma kwa mashirika yanayokuja kufanya uwekezaji wa viwanda ili kumudu ushindani wa soko hilo kimataifa na kuwanufaisha wananchi walio wengi wakiwamo wakulima, wafugaji, wavuvi na wajasiliamali wadogo. Waziri wa Fedha na Mipango, Dr Philip Mpango alitoa wito huo kupitia hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela.

“Iwapo makampuni ya hapa nchini yataweza kutoa huduma ya bima katika uwekezaji mkubwa unaotarajiwa kufanyika nchini ni wazi kuwa licha ya kukuza biashara, kuongeza ajira lakini faida kubwa itabaki Tanzania na hayo ndiyo matarajio ya Rais wetu John Magufuli”, alisema.

Kamishna wa Bima nchini, Dr Baghayo Saqware alisema ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kufanyika nje ya Dar es salaam tangu mwaka 1987 na kwamba itakuwa ikifanyika mikoani lengo likiwa ni kufuata karibu fursa za kiuchumi ziliko. Alisema wadau wa sekta ya bima walioshiriki mkutano huo pia waliweza kutembelea kiwanda cha saruji cha Rhino, Mapango ya amboni na hospitali ya bombo ambako walitoa msaada kwa wagonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela akifungua mkutano mkuu wa 20 wa siku ya bima nchini uliofanyika mwisho wa wiki jijini Tanga. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania ambapo mada kuu ya mwaka huu ilikuwa ni “Bima – Nguzo ya Viwanda”.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (kulia) akifurahia tuzo ya shukurani aliyopewa na Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania, Rukia Adamu (kushoto) kama utambuzi wa mchango wa Serikali katika sekta ya bima katika mkutano wa 20 wa siku ya bima nchini uliofanyika mwishoni wa wiki jijini Tanga.
Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima, Rukia Adamu akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 20 wa siku ya bima nchini uliofanyika mwisho wa wiki jijini Tanga.
Wadau mbalimbali wa sekta ya bima wakifwatilia kwa makini mkutano wa 20 wa siku ya bima nchini uliofanyika mwisho wa wiki jijini Tanga. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania ambapo mada kuu ya mwaka huu ilikuwa ni “Bima – Nguzo ya Viwanda”.
Wadau mbalimbali wa sekta ya bima wakifwatilia kwa makini mkutano wa 20 wa siku ya bima nchini uliofanyika mwisho wa wiki jijini Tanga. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania ambapo mada kuu ya mwaka huu ilikuwa ni “Bima – Nguzo ya Viwanda”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad