Friday, June 26, 2015

UONGOZI WA WIZARA YA UCHUKUZI WAKUTANA NA UJUMBE KUTOKA UWANJA WA NDEGE WA GUANG DONG WA NCHINI CHINA LEO ASUBUHI WIZARANI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanja cha Ndege cha Guang Dong cha nchini China, Bw. Wen Wenxing (kushoto), akimpatia zawadi Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire, leo asubuhi baada ya ugeni huo kukutana na uongozi wa Wizara ya Uchukuzi leo asubuhi.
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanja cha Guang Dong cha nchini China, Bw. Wen Wenxing wakati ujumbe huo ulipokutana na uongozi wa Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa uongozi wa Wizara na ujumbe kutoka Kiwanja cha ndege cha Guang Dong kutoka nchini China, wakati ulipotembelea Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi. Ujumbe umeonyesha nia kuwekeza katika Viwanja vya Ndege vya Tanzania.
(Habari Picha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)     

No comments:

Post a Comment