
Familia ya marehemu Dr. Albert Chagula wa Chang’ombe maduka mawili inawatangazia kuondokewa na mama yetu mpendwa Mwl. Magdalena Chagula kilichotokea ghafla usiku wa juzi tarehe 24.06.2015. Msiba uko nyumbani kwetu Chang’ombe Maduka mawili mtaa wa Majimaji.
Maziko yanatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi tarehe 27.06.2015 majira ya saa tisa alasiri katika makaburi ya Kinondoni, kabla ya mazishi kutakuwa na misa ikifuatiwa na shughuli ya kuaga mwili wa marehemu zitakazoanza majira ya saa tatu asubuhi hapo kesho.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
No comments:
Post a Comment