
Mkurugenzi wa Matekelezo na Uandikishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Lightness Mauki (kulia) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipotembelea Banda la SSRA wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Matekelezo na Uandikishaji Bi. Lightness Mauki akikabidhi zawadi kutoka SSRA kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue baada ya kutembelea banda la SSRA.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Kushoto ni Mkurugenzi wa Matekelezo na Uandikisha akifuatiwa na Afisa Utafiti na Sera Bw.Simon Aikambe.

Maafisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) wakisikiliza maswali na maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi waliotembelea Banda la SSRA katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Mkurugenzi wa Tafiti na Sera Bw. Ansgar Mushi akitoa maelezo juu ya utendaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwa waandishi wa Habari waliofika katika Banda la Mamlaka katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, kushoto ni Afisa Habari Bi. Agnes Lubuva.

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) wakihudumia wananchi waliotembelea katika Banda la Mamlaka katika Maonesho ya Utumishi wa Umma Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam.

Wafanyakazi wa Mamlaka wakiwa wameshikilia vyeti vya tuzo mbalimbali baada ya Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
No comments:
Post a Comment