Askofu
Solomon Mwagisa ambaye ni katibu wa mkutano wa Amani na Upendo
utakaofanyika leo jijini Arusha katika viwanja vya reli kwanzia saa 8
mchana hadi saa 12 jioni akielezea namna walivyojiandaa na mkutano
huo,kushoto ni Askofu Mkuu wa makanisa ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini
kati Solomon Massangwa(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Askofu
Mkuu wa makanisa ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini kati Solomon Massangwa
akizungumza na wanahabari jana jijini hapa kuhusu mkutano huo mkubwa wa
Amani na Upendo ambapo alisema kuwa ni muhimu kwa kila mtu kuhakikisha
Amani inakuwepo huku akisisitiza kuwa bila Amani hakuna kitu chochote
kinachoweza kufanyika pasipo Amani
Paul
Malisa mwakilishi wa Askofu mkuu Josephat Lebulu wa kanisa Katoliki
Arusha ,Paroko wa Parokia ya mtakatifu Theresia Arusha mjini akizungumza
na wanahabari juu ya mkutano huo ambapo alisema kazi walionayo ni
kuhakikisha wanapigia debe Amani hasa katika kipindi hichi kuelekea
uchaguzi mkuu
Eng.Tunzo
Muzava ambaye ni mratibu wa mkutano huo akizungumza na vyombo vya
habari jana alisema kuwa Muhubiri mkubwa wa kimataifa kutoka Marekani
Will Graham anatarajiwa kuhubiri katika mkutano huo huku kwaya zaidi ya
200 kutumbuiza,Mkutano huo unashirikisha makanisa yote ya Arusha
No comments:
Post a Comment