Saturday, June 27, 2015

KONGAMANO LA VIJANA WA KIISLAMU LILILOFANYIKA LEO KATIKA MSIKITI WA FOREST JIJINI MBEYA..

Ustadh Pembe akitoa neno katika Kongamano la vijana  wa kiislamu lililoanza rasmi leo jijini mbeya kwa kuwasihi vijana kulingania dini  ya kiislamu juu ya kumcha mwenyezi mungu na kuwataka vijana kutenda mambo mema, kuachana na mambo yasiyo fahaa na yanayo katazwa katika dini ya kiislamu, licha ya hayo Ustadh Pembe alizungumzia mambo yanayotakiwa kufanyika hasa katika mwezi mtukufu wa ramadhani ikiwemo, kuswali, kutoa zaka, na kutenda mambo yanayo mpendeza mwenyezi mungu...PICHA ZOTE NA (FADHIRI ATICK) MBEYA.
"Vijana ndio nguvu kazi katika taifa, hivyo basi tujitahidi kukumbuka hadithi mbalimbali za mitume jinsi ambavyo zinasisiutiza kumcha mwenyezi mungu"
Ustadh Ibrahimu nae alikuwepo katika warsha iliyo fanyika leo msikiti wa forest jijini mbeya
Baadhi ya vijana walio hudhuria kongamano hilo..
Kutoka kulia ni Ustadh  Ibrahim na Ustadh Pembe wakitafiti jambo..
Vijana walio hudhuria kongamano hilo lilifanyika katika msikiti wa forest jiji mbeya leo.BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

No comments:

Post a Comment