Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF.Bw. Aloyce Ntukamazina akiwasilisha mada juu ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji katika Mfuko wa GEPF,wakati wa semina kwa Maafisa Rasilimali Watu kutoka Wilaya ya Ilala iliyofanyika kwenye hoteli ya Peacock,jijini Dar es salaam.
Meneja wa GEPF mkoa wa Ilala,Bw Jafari Meraji akisisitiza jambo juu ya faida zipatikanazo katika mpango wa hiari wa kujiwekea akiba (VSRS)
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo Bw Sebastian Enosh ambaye ni Meneja Rasilimali watu kutoka DIT akitoa mchango wake pamoja na ushauri kwa Mfuko wa GEPF.
Pichani baadhi ya washiriki wa semina hiyo maalum wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na maafisa wa GEPF.
Maafisa Rasilimali watu wakipata maelekezo ya kujaza fomu na kujiunga na mpango wa hiari wa kujiwekea akiba kutoka kwa Afisa Masoko wa GEPF Bw Avit Nyambele.

No comments:
Post a Comment