Friday, September 7, 2012

Warembo wa Redd's Miss Kinondoni kuingia Kambini leo

Mratibu wa Shindano la Redd's Miss Kinondoni 2012,Vivian Sirikwa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari na Warembo washiriki wa Shindano hilo (hawapo pichani) katika ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza rasmi kambi ya Redd's Miss Kinondoni inayozinduliwa leo katika ukumbi wa Ambassador Lounge,Jijini Dar.jumla ya washiriki 10 watapanda jukwaani siku ya ijumaa ya Septemba 14,katika ukumbi wa Danken,Mikocheni kuwania taji hilo la Ulimbwende Kinondoni.Kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original,Victoria Kimaro.
 
Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original,Victoria Kimaro akizungumza jambo kwa Warembo washiriki wa Shindano la Redd's Miss Kinondoni (hawapo pichani) wakati wa Mkutano na Wanahabari wa kuwatangaza warembo hao na kuitangaza rasmi kambi ya Redd's Miss Kinondoni inayozinduliwa leo katika ukumbi wa Ambassador Lounge,jijini Dar.jumla ya washiriki 10 watapanda jukwaani siku ya ijumaa ya Septemba 14,katika ukumbi wa Danken,Mikocheni kuwania taji hilo la Ulimbwende Kinondoni.Kushoto ni Mratibu wa Shindano la Redd's Miss Kinondoni 2012,Vivian Sirikwa.
Warembo watakaoshiriki katika Kinyang'anyiro cha Redd's Miss Kinondoni 2012 wakiwa katika picha ya pamoja na Mwalimu wao,Jennifer Kakolaki (katikati) muda mfupi baana ya kutambulishwa kwa Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya JB Belmont,jijini Dar.

No comments:

Post a Comment