Waisilamu
kutoka maeneo mbali mbali ya jijini Dar es Salaam wakishiriki katika
maandamano ya kuelekea Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili
kupariwa ufumbuzi wa juu ya kamata kamata ya Jeshi la Polisi dhidi ya
waisilamu waliokataa kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na
Makazi.Wameendelea na msimamo wa kupingwa kukamatwa wanaokataa
kuhesabiwa Sensa.Jeshi la Polisi limekubali kuwaachia huru waislamu wote
waliokamatwa.Waislamu watangaza ushindi,Wasema Bado Mkuu wa baraza la
Mitihani Joyce Ndalichako ajiandae na maandamano ya namna hiyo hadi
ofisini kwake na baadae Bakwata wanayotaka ifutwe. Muda huu wapo hapa
Msikiti Kichangani,Magomeni wanapanga Mkakati wa kuandaa maandamano
mengine.
Mabango yenye maelezo tofauti tofauti.
Maandamano yakiendelea.
Maandamabo yakiwa yamefika nje ya Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani.
Waisilamu wakiswali sala ya Laasiri, mbele ya Wizara ya mambo ya ndani
wakati wakisubiri viongozi wao waliokwenda kuzungumza na jeshi la polisi
ili kupata ufumbuzi wa juu ya kamata kamata ya jeshi la polisi dhidi ya
waisilamu wanaokataa kuhesabiwa.
Mmoja wa Waislam akiwa amenyanyuliwa juu juu.




No comments:
Post a Comment